The VOP Ministry - Home
 • 19 April SIRI YA KUMSHINDA SHETANI

  SIRI YA KUMSHINDA SHETANI(UFU.3:21) Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi ,kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti changu cha enzi

 • 31 March VIKWAZO KATIKA MAOMBI

  VIKWAZO KATIKA MAOMBITunahitaji kuomba ili tubadilishe maisha yetu, tunahitaji kuomba ili kudhihilisha imani yetu kwa Mungu wetu ambaye tunamtegemea, tunahitaji kuomba ili tupate rehema na neema ya kutuwezesha kuishi maisha matakatifu, tunahitaji kuomba ili tukue kiroho. Lakini vipo vipingamizivikwazo ambavyo vinatokana na sisi wenyewe, ambavyo vinasababisha maombi yetu yasijibiwe. Vikwazo hivyo ni kama vifuatavyo:-

 • 10 March KUNENA KWA LUGHA NINI?

  3. KUNENA KWA LUGHA NINI?Kunena kwa lugha ni kuongea katika Roho, kuomba katika Roho au kuimba katika Roho Roho mtakatifu hutumia kinywa cha mtu kutoa maneno , Maneno yanayotoka hayatoki kwenye akili ya mtu, yanatoka mdomoni tu. Sehemu ya ubongo inayohusika na lugha haifanyi kazi wakati mtu anaponena kwa lugha . Hii inaonyesha kwamba kunena kwa lugha kunaongozwa na Nguvu nyingine ambayo haihusiani na mtu anayenena yaani mwili wake na akili zake . Nguvu hii ndiyo nguvu ya Roho mtakatifu, Roho Mtakatifu hunena kupitia mtu kwa jinsi apendavyo yeye wala hapangiwi kwamba anene hivi au anene vile.

 • 16 February MUHURI WA MUNGU

  Mlokole amepigwa muhuri na MunguMaana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo tena kwa hiyo katika yeye ni Amini Mungu apate kutukuzwa kwa sisi. Basi yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo na kututia mafuta ni Mungu, naye ndiye aliyetutia Muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu. (2 wakorintho1:20-22)Nanyi pia katika huyo Kristo mmekwisha kulisikia Neno la kweli habari njema za wokovu wenu tena mmekwisha kumwamini yeye na kutiwa Muhuri na Roho yule wa ahadi aliye mtakatifu ndiye aliye arabuni ya urithi wetu ili kuleta ukombozi wa milki yake kuwa sifa ya utukufu wake. (Efe 1:13-14)

 • 16 February Wokovu unampa mtu mamlaka ya Kimungu juu ya ufalme wa Shetani

  Wokovu unampa mtu mamlaka ya Kimungu juu ya ufalme wa Shetani. Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia nilimwona Shetani akianguka kutoka Mbinguni kama umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yale adui wala hakuna kitu kitachowadhuru.(luka 10:17-19)Utawakanyaga simba na nyoka mwana - simba na joka utawaseta kwa miguu.(zaburi 91:13)Aaminiye na kubatizwa ataokoka asiyeamini, atahukumiwa na ishara hizo zitafuatana na hao waaminio kwa jina langu watatoa pepo watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya. (Marko 16:16-18)